KIPENGA CHA SHANGILIKA 2026 CHAPIGWA

Na Winifrida Makwega – Iringa

 

Jijini Arusha, tarehe 5 Julai 2026, kunatarajiwa kufanyika tamasha kubwa la kwaya za Kikristo la kusifu na kumtukuza Mungu, linalofahamika kama SHANGILIKA 2026.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia dawati la Mwanakwetu mapema tarehe 28 Juni 2026, tamasha hili linatarajiwa kukutanisha kwaya mbalimbali kutoka mikoa tofauti ya Tanzania.

 

Baadhi ya kwaya zitakazoshiriki ni pamoja na:

Eden Moravian Choir (Arusha), El Shaddai Choir (Dodoma), Paradise Moravian Choir (Mbeya), Upendo Choir (Arusha), Moravian Efatha Choir (Dar es Salaam), Tumaini Shangilieni Choir (Arusha), pamoja na kwaya nyingine nyingi.

 

Tamasha hili litafanyika siku ya Jumapili, tarehe 5 Julai 2026, katika Kanisa la Anglikana – Saint James, Kaloleni, Arusha.

 

Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa waandaaji alisema:



“Hatuji kumtafuta mshindi, bali njoo nyote tumsifu na kumtukuza BWANA, maana mshindi tangu zamani ni Yesu Kristo.”

 

Hii ni fursa ya kipekee kwa Wakristo na jamii kwa ujumla kushiriki katika ibada ya pamoja ya sifa na kuimarisha umoja wa kiroho kupitia muziki wa injili.

Waumini wote mnakaribishwa kuhudhuria na kushiriki katika tukio hili la baraka.

Karibuni wote tushangilie pamoja katika Bwana!

 










0/Post a Comment/Comments