✍️ Emmanuel Masuza
Mwanakwetu Sports.
Moja ya viungo bora kuwahi kuubariki mpira wa miguu duniani,World Cup ya 2014 iliyofanyika Brazil ilikuwa ya kwanza kwa Paul Pobga na alifanikiwa kuibuka na tuzo ya mchezaji bora kijana wa mashindano,kisha akafanikiwa tena kuwa sehemu ya wachezaji muhimu walioiwezesha Ufaransa kutwaa World Cup 2018.
Mara baada ya Pobga kupata mafanikio hayo makubwa akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa,muda mfupi baadaye Pobga alianza kuandamwa na majeraha,migogoro ya familia pamoja na kesi,changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zilimtoa Paul Pobga katika soka la ushindani.
Kwa sasa amerejea kwenye soka la ushindani baada ya kukosekana kwa muda mrefu na nyakati hizi yupo na AS Monaco ya Ufaransa,na msimu uliotoka kumalizika alipata dakika chache za kucheza na kama ulipata nafasi ya kumshuhudia ni wazi kuwa dunia inapaswa kukubali kuwa Paul Pobga siyo yule aliyekuwa amezoeleka na kama hukumshuhudia vizuri akiwa kwenye ubora wake ni wazi kuwa hautopata nafasi hiyo tena na unapaswa kujilaumu si kwa sababu hakuna viungo wengine duniani wanaoweza kukupa burudani ya soka bali ni kwa sababu hukumuona Paul Labile Pobga.

Post a Comment