Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Hali ya sintofahamu imeendelea kuelekea michuano ya Kombe la Dunia 2026 baada ya mwamuzi wa Somalia, Omar Artan, kuripotiwa kuzuiwa kuingia Marekani, jambo lililoibua mjadala mkubwa katika dunia ya soka.
Aliyekuwa mshambuliaji wa England, Ian Wright, ameikosoa Marekani kufuatia tukio hilo huku akidai kuwa maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea kugubikwa na changamoto mbalimbali.
Wright alisema taarifa za watu kuzuiwa kuingia Marekani zimekuwa zikiongezeka kila siku, zikihusisha mashabiki, wachezaji, maofisa, waandishi wa habari na sasa waamuzi.
“Nimesoma kuwa mwamuzi kutoka Somalia amezuiwa kuingia Marekani na Kila baada ya saa chache kuna taarifa nyingine za mashabiki kuzuiwa, wachezaji kuzuiwa, maofisa kuzuiwa, waandishi wa habari kuzuiwa , sasa hata waamuzi,” alisema Wright.
Mbali na hilo, Wright alieleza kuwa gharama za tiketi, malazi na usafiri zimeendelea kupanda na kuongeza maswali kuhusu maandalizi ya mashindano hayo makubwa duniani.
“Tiketi zimekuwa ghali sana, malazi ni ghali na gharama za usafiri zimepanda. Je, hivi ndivyo wenyeji wanavyopaswa kuendesha mashindano makubwa kama haya?” alihoji.
Nyota huyo wa zamani pia alilinganisha hali hiyo na namna Qatar ilivyokosolewa kabla ya Kombe la Dunia la mwaka 2022, akidai kuwa Marekani haijakosolewa kwa kiwango sawa licha ya changamoto zinazoendelea kujitokeza.
“Hili sio tu Kombe la Dunia, ni Kombe la Dunia la vurugu. Timu itakayoshinda italazimika kupitia mazingira magumu ili kufikia mafanikio,” alisema Wright.
Mpaka sasa, timu zinazo wasili nchini Marekani zimekabiliwa na ukaguzi mzito , wengine wamekaguliwa bila kujali hadhi Yao , ni kweli jambo hili halijakaa sawa.
Kwa upande mwingine sababu ya haya yote kutokea huenda ni sababu za kisiasa ambapo kwa siku za karibuni Marekani iliingia kwenye vita dhidi ya Iran , hivyo hatua hiyo huenda ni mpango mkakati wa Taifa ili kuhakikisha nchi inakuwa salama kwenye kipindi Cha mashindano ambapo watu kutoka mataifa mbali mbali watakuwa nchini humo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment