Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports
Kiungo mshambuliaji wa Singida Black Stars, Mossi Nduwumwe, amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu (hatrick) katika msimu wa 2025/26 wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuiongoza timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mzunguko wa 27 wa ligi hiyo.
Nduwumwe, raia wa Burundi, alifunga mabao hayo matatu katika mchezo huo na kuisaidia Singida Black Stars kupata alama tatu nakuendelea kujikita nafasi ya nne wakiwa na alama 47 wakizidi kujihakikishia nafasi ya kucheza kombe la shirikisho msimu ujao.
Kutokana na mabao hayo, Nduwumwe amefikisha mabao 12 msimu huu na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi akiwa nyuma ya Feisal kiungo mshambuliaji wa Azam mwenye mabao 14.
Aidha, hatrick ya Nduwumwe imekuwa ya kwanza kushuhudiwa tangu kuanza kwa msimu wa 2025/26, hatua inayomweka katika rekodi za mwanzo za ushindani wa ufungaji mabao katika ligi hiyo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment