Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Canada Jonathan David amefunga mabao matatu katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Kundi B dhidi ya Qatar, ambapo Canada iliibuka na ushindi wa mabao 6-0.
Katika mchezo huo Canada walitawala mchezo kwa muda mwingi , Jonathan David alifunga mabao hayo matatu dakika ya 29, 45+3 na 90+2, Baada ya matokeo hayo, Canada imeendelea kuimarisha nafasi yake ya kufuzu 32 bora wakiongoza kundi wakiwa na alama nne.
Kwa matokeo hayo, Jonathan David anakuwa mchezaji wa pili kufunga hat trick katika mashindano hayo, baada ya Lionel Messi kufanya hivyo katika mchezo wa Argentina dhidi ya Algeria.
Kwa sasa, Jonathan David anaongoza orodha ya wafungaji bora wa mashindano hayo akiwa na mabao sawa na Lionel Messi huku michezo mingine ya hatua ya makundi ikiendelea.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment