“HAPA GEN Z ULIKUWA NA MIAKA MINGAPI”

✍️ Emmanuel Masuza 

Mwanakwetu Sports 

Ilikuwa mwaka 2010 pale katika Ardhi ya Wajukuu wa Madiba ilipigiwa mechi ya kwanza ya Ufunguzi ya kombe la Dunia lililofanyika AFRIKA KUSINI ikiwa ni mara ya kwanza tangu Dunia kuubwa kombe hili kufanyika ndani ya Afrika, Bara lililobarikiwa wingi wa utajiri wa rasilimali zikiwemo Milima na Hifadhi nzuri za Wanyama pori. Nchi za afrika zilizopata nafasi ya kushiriki kombe lile wakati ule yalikuwa ni mataifa sita tu kutoka ukanda wa Afrika ilikuwa ni GHANA,SOUTH AFRICA, ALGERIA, TUNISIA, NIGERIA, CAMEROON na kushuhudia timu ya taifa ya Ghana ikaweka historia kwa mara ya kwanza kutoka ukanda wa Afrika kuishia hatua ya Robo fainali tangu Mashindano hayo kuanziashwa kabla ya Timu ya taifa ya Morocco kuja kuvunja rekodi hiyo pale mwaka 2022 Baada ya kufika hadi nusu fainali kwa kuwatoa timu ya taifa ya Ureno katika kombe la dunia lililofanyika pale URUSI,Ureno wakiwa na mastaa wakubwa wa soka duniani wakiwemo akina Cr7 (Christiano Ronaldo),Bernado silva na kadharika.

Mechi ile ya Ufunguzi iliwakutanisha AFRIKA KUSINI (BAFANABAFANA) dhidi ya Mexico na mchezo kutamatika kwa sare ya 1-1, ilikuwa ni historia kubwa kwa timu ya taifa ya South Africa, timu ile ikiwa na kizazi za dhahabu wakiwemo akina Steven Pienaar ,Siphiwe Tshabalala, Aaron Mokoena,Itumeleng Khune, Katlego Mphela wakiwa chini ya kocha Carlos Alberto Parreira “GEN Z WENGI MLIKUWA BADO WADOGO SANA”

Waswahili wanasema “DAWA YA MOTO NI MOTO” Historia inaenda kuandikwa tena safari hii sio tena Afrika wala ulaya ni kule Amerika, ni mataifa matatu ambayo ni USA, CANADA pamoja na MEXICO ndizo zinaandaa Michuano hii, Mchezo wa kwanza wa ufunguzi utapigwa kule Mexico na utawakutanisha tena AFRIKA KUSINI dhidi ya MEXICO zamu hii sio tena Tshabalala wala steve pienaar ni kizazi kipya cha BAFANABAFANA kilicho jaa nyota wadogo wakiwemo akina Ronwen Williams, Relebohile Mafokeng bila kumsahau teboho Mukoena, Awamu hii ni mataifa kumi kutoka Afrika yanashiriki Michuano hiyo mikubwa duniani, mataifa hayo ni AFRIKA KUSINI, SENEGAL, GHANA, EGYPT(MISRI), DR CONGO,ALGERIA, MOROCCO, CAPE VADE, IVORY COST pamoja na TUNISIA “GEN Z MPOOO?


0/Post a Comment/Comments