Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limethibitisha kuwa mwamuzi wa Somalia, Omar Abdulkadir Artan, atalipwa stahiki zote za Kombe la Dunia 2026 licha ya kutoshiriki mashindano hayo baada ya kuzuiwa kuingia nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Artan atapokea ada ya mashindano, posho na bonasi zote zinazotolewa kwa waamuzi wa Kombe la Dunia sawa na waamuzi wengine waliopo kwenye michuano hiyo.
Artan alikosa nafasi ya kuchezesha Kombe la Dunia baada ya kuzuiwa kuingia Marekani alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
Uamuzi wa FIFA unamaanisha kuwa mwamuzi huyo hataathiriwa kifedha na tukio lililomzuia kushiriki michuano hiyo, huku akiendelea kunufaika na haki zote alizostahili kama sehemu ya waamuzi walioteuliwa kwa Kombe la Dunia 2026.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment