Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Yan Diomandé, amefikia makubaliano ya masharti binafsi ya kujiunga na Paris Saint-Germain (PSG), hatua inayoiweka klabu hiyo ya Ufaransa karibu na kukamilisha usajili wake katika dirisha hili la usajili.
Mchezaji huyo amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ligue 1na UCL , baada ya kuichagua PSG licha ya kuwapo kwa maslahi kutoka kwa baadhi ya klabu za Ligi Kuu England ikiwemo Liverpool.
Hata hivyo, uhamisho huo bado haujakamilika kwa kuwa PSG na RB Leipzig wanapaswa kufikia makubaliano kuhusu ada ya usajili, Leipzig inadaiwa kutaka zaidi ya euro milioni 100 ili kumruhusu mchezaji huyo kuondoka.
Awali, Liverpool iliwasilisha ofa ya euro milioni 90 pamoja na nyongeza ya euro milioni 10, lakini pendekezo hilo lilikataliwa na Leipzig, Hali ambayo inaendelea kusimamia thamani yake katika mazungumzo ya uhamisho.
Wakati huohuo, Leipzig imependekeza utaratibu ambao ungemruhusu Diomandé kusajiliwa na PSG katika dirisha hili la usajili, kisha aendelee kuichezea klabu hiyo ya Ujerumani kwa mkopo hadi mwanzoni mwa msimu wa 2027/28.
Kwa sasa, hatua ya mwisho ya uhamisho huo inategemea makubaliano kati ya PSG na RB Leipzig kuhusu ada ya usajili na masharti mengine ya dili hilo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment