Almirón aandika historia kwa kadi nyekundu ya kwanza chini ya “Sheria ya Prestianni”

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kiungo na nahodha wa Paraguay, Miguel Almirón, amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kupewa kadi nyekundu chini ya sheria mpya ya FIFA inayojulikana kama “Prestianni Law”, baada ya kufunika mdomo wake wakati akizungumza na beki wa Uturuki Mert Muldur kwenye mchezo wa Kundi D wa Kombe la Dunia 2026 uliomalizika kwa Paraguay kushinda 1-0.

Tukio hilo lilitokea katika dakika 45+3 wakati wa mabishano kati ya wachezaji hao wawili, baada ya waamuzi wa VAR kupitia picha za tukio hilo, mwamuzi Ivan Barton aliamua kumuonyesha Almirón kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kukiuka kanuni mpya inayowazuia wachezaji kufunika midomo yao wanapozungumza na wapinzani katika mazingira ya mabishano. 

Sheria hiyo ilianzishwa na FIFA kufuatia sakata lililomhusisha mchezaji wa Benfica, Gianluca Prestianni, ambaye alituhumiwa kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya Vinicius Junior wa Real Madrid huku akiwa amefunika mdomo wake, jambo lililofanya iwe vigumu kuthibitisha kilichosemwa. Kutokana na tukio hilo, mamlaka za soka zikaamua kuanzisha adhabu kali kwa wachezaji wanaoficha midomo yao wakati wa mabishano uwanjani. 

 Kadi hiyo nyekundu ya Almirón imekuwa moja ya matukio makubwa yaliyoibua mjadala katika Kombe la Dunia 2026, ikiwa ni mara ya kwanza sheria hiyo mpya kutumika katika mashindano rasmi ya FIFA. 

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com





0/Post a Comment/Comments