Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mataifa tisa ya Afrika yamefanikiwa kufuzu hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kumalizika kwa michezo ya hatua ya makundi, huku Tunisia ikiwa timu pekee ya bara hilo iliyoshindwa kusonga mbele.
Mataifa yaliyofuzu ni Morocco, Afrika Kusini, Ivory Coast, Misri, Cape Verde, Senegal, Ghana, Algeria na DR Congo. Awali Afrika ilikuwa na wawakilishi 10 katika mashindano hayo, lakini matokeo ya hatua ya makundi yameifanya idadi hiyo kupungua kwa timu moja.
Hatua ya 32 Bora inaanza Juni 28, 2026, ambapo Afrika Kusini itakuwa timu ya kwanza ya Afrika kushuka dimbani dhidi ya wenyeji Canada, ratiba hiyo itaendelea hadi Julai 4, 2026, itakapohitimishwa na mchezo kati ya Ghana dhidi ya Colombia.
Katika kipindi hicho, mataifa mengine ya Afrika yataendelea na mechi zao za mtoano yakisaka nafasi ya kuwapeleka hatua ya 16 Bora ya mashindano hayo.
Kufuzu kwa mataifa tisa kunamaanisha Afrika imeendelea kuwa na idadi kubwa ya wawakilishi katika hatua ya mtoano, huku kila timu ikiwa na nafasi ya kuendeleza safari yake kuelekea hatua za mwisho za michuano hiyo.
Matokeo ya hatua ya 32 Bora yataamua ni mataifa mangapi ya Afrika yatakayovuka kwenda hatua ya 16 Bora na kuendelea kuliwakilisha bara hilo katika mbio za kuwania taji la Kombe la Dunia 2026.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com


Post a Comment