Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Miamba ya soka nchini England, Chelsea FC wanatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho za kumtangaza Xabi Alonso kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya karibu na klabu hiyo zinaeleza kuwa mazungumzo kati ya pande zote mbili yamekamilika na kocha huyo tayari amekubali kuinoa timu hiyo kuelekea msimu ujao wa mashindano.
Xabi Alonso anatajwa kuvutiwa na mradi wa muda mrefu wa Chelsea pamoja na mpango wa kuijenga upya timu hiyo ili kurejea kwenye ushindani mkubwa ndani ya Premier League na michuano ya Ulaya.
Kocha huyo raia wa Hispania ameendelea kupata sifa kubwa barani Ulaya kutokana na mafanikio yake ya ukocha katika misimu ya hivi karibuni, hali iliyowafanya viongozi wa Chelsea kumuona kama chaguo sahihi la kuiongoza klabu hiyo.
Utambulisho rasmi wa kocha huyo unatarajiwa kufanyika hivi karibuni baada ya klabu kukamilisha taratibu za mwisho za kimkataba.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment