WANANCHI WATIMUA KOCHA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Uongozi wa Young Africans Sports Club umetangaza kumfuta kazi Kocha Mkuu wa kikosi cha hicho, Pedro Goncalves, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 6, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, klabu imesema imefikia uamuzi huo baada ya tathmini ya ndani ya mwenendo wa timu, Uongozi pia umemshukuru kocha huyo kwa mchango wake katika kipindi alichohudumu na kumtakia mafanikio katika majukumu yake yajayo.

Klabu imeeleza kuwa kikosi kitaongozwa na Abdihamid Moalin kwa kushirikiana na Patrick Mabedi hadi mwisho wa msimu.

Hatua hiyo inakuja wakati msimu ukiendelea, huku uongozi haujaeleza kuhusu mpango wa kumpata kocha mkuu mpya.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments