Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kukosekana kwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta pamoja na baadhi ya wachezaji wenye uzoefu mkubwa ndani ya kikosi hicho, kumefungua ukurasa mpya kwa nyota wengine kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wao na kuanza safari ya kulitumikia taifa kwa kiwango kikubwa zaidi.
Kikosi kilichoitwa ni kwaajili ya maandalizi kuelekea michezo ya kirafiki kalenda ya fifa ambayo itapigwa mwezi Juni 2026 , Stars watacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Rwanda na Uganda.
Samatta ambaye ameendelea kukosekana tangu michezo ya FIFA Series iliyofanyika Rwanda, ameungana na majina mengine yenye uzoefu kama , Zimbwe Jr, Kapombe, Kibu Denis, Idd Nado na Kagoma ambao hawapo kwenye kikosi cha sasa cha Stars, hali hiyo imeibua mjadala mkubwa kwa mashabiki, lakini pia imeonekana kuwa mwanzo wa Enzo mpya ndani ya timu ya taifa.
Benchi la ufundi linaonekana kuelekeza nguvu katika kujenga kizazi kipya cha wachezaji watakaokuja kuibeba Taifa Stars kwa miaka ijayo, Wachezaji wengi waliokosekana ni wale waliolitumikia taifa kwa muda mrefu na sasa nafasi zao zinaanza kujazwa na damu changa zenye njaa ya mafanikio, jambo ambalo linaweza kuleta ushindani mkubwa ndani ya kikosi.
Kupitia mabadiliko hayo, vijana wanaopata nafasi wanatarajiwa kujifunza mapema mazingira ya soka la kimataifa, kuongeza uzoefu na kuijenga timu yenye ushindani kuelekea michuano mikubwa ijayo ikiwemo AFCON 2027.
Ingawa mashabiki wataendelea kuwakumbuka wakongwe hao, hatua hii inaweza kuwa mwanzo wa zama mpya za mafanikio kwa Taifa Stars ikiwa vipaji vipya vitaendelea kuaminiwa na kupewa muda wa kukua.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment