Wachezaji wa United waomba Carrick apewe mkataba wa kudumu

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Baadhi ya wachezaji waandamizi wa klabu ya Manchester United wanatajwa kutaka kocha wao wa muda Michael Carrick apewe nafasi ya kuendelea kuinoa timu hiyo baada ya kuonyesha mabadiliko makubwa ndani ya kipindi kifupi ndani ya timu hiyo.

Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa nahodha Bruno Fernandes, Harry Maguire, Matheus Cunha pamoja na kiungo chipukizi Kobbie Mainoo ni miongoni mwa nyota wanaomuunga mkono Carrick kuendelea kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho.

Carrick ameirejesha United kwenye ushindani mkubwa wa ligi, huku timu hiyo ikikusanya alama 42 tangu achukue mikoba ya kuinoa timu, rekodi inayowafanya kuwa miongoni mwa timu bora zaidi ndani ya kipindi hicho.

Mbali na ubora huo wa matokeo, Carrick ameisadia United kufuzu michuano ya UEFA Champions League kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitatu, hatua iliyoongeza imani kwa wachezaji na mashabiki kuwa anaweza kuwa chaguo sahihi la muda mrefu.

Pamoja na mafanikio hayo, mabosi wa United wanatajwa kuendelea kufanya mazungumzo na makocha wengine kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho, lakini Carrick anaonekana kuwa mbele kwenye mbio hizo kutokana na sapoti kubwa anayopata kutoka kwenye kikosi chake.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments