WACHEZAJI MADRIDI WAZICHAPA MAZOEZINI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Viungo wa Real Madrid, Aurelien Tchouameni na Federico Valverde wameingia kwenye ugomvi mwingine ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo vya klabu hiyo kufuatia kutokuwa na maelewano baina Yao.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, tukio hilo limetokea baada ya mazoezi ya timu, huku Valverde akipelekwa hospitalini kwa uchunguzi baada ya kupata majeraha kufuatia kupigwa ngumi wakati wa ugomvi huo, Hata hivyo, bado haijaelezwa rasmi chanzo cha mvutano huo kati ya wachezaji hao wawili.

Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa uongozi wa Real Madrid unatarajia kuchukua hatua dhidi ya wachezaji hao kufuatia matukio yanayoelezwa kujirudia ndani ya kikosi hicho katika siku za karibuni.

Real Madrid inaendelea na maandalizi ya michezo yake ijayo huku sakata hilo likiendelea kuzua mjadala kuhusu hali ya nidhamu ndani ya timu kuelekea hatua za mwisho za msimu .

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments