WAAMUZI WAPENDEZESHA DABI YA KARIAKOO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezo wa Dabi ya kariakoo ulipigwa kwenye dimba la Meja jeneral Isamuhyo umetamatika kwa miamba hiyo ya soka Simba na Yanga kutoshana nguvu ya 2-2 kwenye mchezo ulijaa ufundi na mbinu kutoka pande zote mbili.

michezo ya hivi karibuni iliyo wakutanisha miamba hao imekumbwa na lawama kutoka kwa wadau na mashabiki wakishindwa kuridhika na maamuzi ya waaamuzi wa ndani kutokana na kushindwa kutafsiri matokeo ambayo mara nyingi huathiri matokeo ya mchezo.

Waamuzi kutokea nchini Morocco wakiongozwa na Hamza El Fareq ambaye alikuwa mwamuzi wa kati pia ni miongoni mwa waamuzi watakao husika kwenye fainali za kombe la Dunia akiwa kwenye upande wa mwamuzi msaidizi wa VAR.

Kwenye mchezo huo, waamuzi wamekuwa na utendaji mzuri kwa dakika zote tisini wakitafsiri Sheria kwa haki bila kutumia upande wowote na kumaliza mchezo bila kuacha maswali na malalamiko baada ya mchezo.

Waamuzi wa Tanzania wnatakiwa kujifunza kutoka kwa waamuzi wenzao wenye uzoefu ili kuepuka makosa ya kibinadamu yanayo gharimu matokeo ya upande mmoja.

Kwa ujumla , waamuzi wameutendea haki hivyo ni jukumu la bodi ya ligi kuendelea kuchukua waamuzi kutoka nje ya Tanzania kwenye mchezo huu ili kuepuka malalamiko

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments