VICTOR UDOH AFARIKI DUNIA SUMU IKITAJWA KUCHUKUA UHAI WAKE

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Simanzi kubwa imegubika familia, marafiki na wadau wa soka baada ya taarifa za kifo cha mchezaji kijana Victor Udoh kuzua majonzi makubwa nchini Nigeria, Nyota huyo aliyewahi kutumikia timu za Southampton na Royal Antwerp ameripotiwa kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 21.

Victor Udoh alizaliwa Oktoba 18, 2004, amefariki usiku wa tarehe 25 mei 2026, alikuwa akitajwa kuwa mmoja wa vijana wenye ndoto kubwa katika dunia ya soka. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya nchini Nigeria, mchezaji huyo alikuwa jijini Abuja akiwa na marafiki zake usiku mmoja kabla ya kukutwa amefariki katika mazingira yanayodaiwa kuhusishwa na sumu ya chakula.

Kifo chake kimeacha majonzi makubwa kwa mashabiki wa soka walioamini kuwa kijana huyo alikuwa bado ana safari ndefu ya mafanikio mbele yake, Ndoto zake za kung’ara barani Ulaya zimekatishwa ghafla akiwa katika umri mdogo.

Hakika maisha ni mafupi na yasiyotabirika. Victor Udoh ameondoka duniani mapema mno, lakini jina lake litaendelea kukumbukwa na wale wote walioguswa na kipaji chake. Apumzike kwa amani.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments