VALVERDE, TCHOUAMENI WAPIGWA FAINI YA SH BILIONI 1.5

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Wachezaji wa Real Madrid, Federico Valverde na Aurelien Tchouameni, wamepigwa faini ya euro 500,000 kila mmoja, sawa na bilioni 1.5 za Tanzania, baada ya klabu hiyo kukamilisha uchunguzi wa ndani kuhusu tukio lililosababisha kufunguliwa kwa taratibu za kinidhamu dhidi yao.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ilieleza kuwa wachezaji hao walifika mbele ya uongozi wa timu na kukiri kilichotokea huku wakiombana radhi.

Mbali na hilo, wawili hao waliomba radhi kwa klabu, benchi la ufundi, wachezaji wenzao na mashabiki wa timu hiyo, huku wakieleza utayari wa kushirikiana na uongozi wa Real Madrid katika hatua zote zilizochukuliwa.

Kutokana na maelezo hayo, klabu hiyo imeeleza kuwa haitachukua hatua nyingine za kimichezo dhidi ya viungo hao zaidi ya adhabu ya kifedha iliyotolewa.

Hivyo, uamuzi huo unahitimisha rasmi mchakato wa ndani wa kinidhamu uliokuwa ukiwahusu wachezaji hao ndani ya kikosi hicho.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments