Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shabiki wa Manchester United, Frank Ilett, atalazimika kuendelea kubaki na nywele zake baada ya timu hiyo kushindwa kuifikia ushindi wa michezo mitano mfululizo msimu huu.
Frank Ilett aliweka ahadi ya kutonyoa nywele mpaka Manchester United ishinde michezo mitano mfululizo, jambo lililogeuka gumzo miongoni mwa mashabiki wa soka ulimwenguni .
Baada ya United kupata ushindi katika michezo mitatu mfululizo, matumaini ya shabiki huyo yalionekana kurejea huku mashabiki wakianza kuamini huenda ahadi yake ikafikia mwisho kabla ya msimu kumalizika.
Hata hivyo, sare ya 0-0 dhidi ya Sunderland katika mchezo wa nne wa mfululizo imezima ndoto hizo na kuifanya United kushindwa kufikisha ushindi tano mfululizo.
Hivyo, Kutokana na timu hiyo kubakiwa na michezo miwili pekee kabla ya msimu kumalizika, Frank Ilett sasa atalazimika kusubiri hadi msimu ujao kuona kama ataweza kutimiza ahadi yake ya kunyoa nywele.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment