UNITED KUSHIRIKI UEFA MSIMU UJAO

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Manchester united imekata tiketi kushiriki michuano ya UEFA Champions league kwa msimu ujao wa 2026/2027, ushindi wa 3-2 katika dimba la Old Trafford ndio inahakikisha nafasi ya United kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Kwa matokeo hayo, United wanasalia nafasi ya tatu wakiwa na alama 64 na michezo 35, huku wakisalia na michezo mitatu ambayo kwa idadi ya alama walizivuna zinawapa tiketi ya kufuzu wakiungana na Arsenal na City ambao tayali wameshafuzu.

Ikumbukwe kuwa, mara ya mwisho kwa mashetani kushiriki UCL ni msimu wa 2023/2024 ambapo waliondolewa mapema hatua ya makundi ambapo kundi lao lilijuimuisha miamba kama vile Bayern Munich, Copenhagen na Galatasaray.

Macho na masikio yanaelekezwa kuanzia kwenye msimu wa usajili ili kuangalia ni vyuma gani vita mwaga wino kuipeperusha bendera ya nyekundu na nyeupe kwenye kuitetea heshima ya klabu iliyopotea kwa misimu kadhaa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments