TIMU NI KUBWA KULIKO MCHEZAJI

 

Mwanakwetusports.

Katika mchezo wa mpira wa miguu duniani kote, nidhamu imeendelea kuwa moja ya misingi muhimu ya mafanikio ndani ya timu, Klabu nyingi zimekuwa zikichukua hatua dhidi ya wachezaji wanaokiuka maadili na taratibu za timu kwa lengo la kulinda umoja na mazingira ya ushindani ndani ya kikosi.

Katika Ligi Kuu Tanzania Bara, matukio ya aina hiyo yamewahi kujitokeza mara kadhaa ambapo baadhi ya wachezaji waliondolewa au kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na mienendo isiyofaa ndani ya klabu.

Simba SC ni miongoni mwa klabu zilizowahi kuchukua maamuzi hayo kwa wachezaji wake muhimu akiwemo Kiungo na nahodha Jonas Mkude ambaye alihusishwa na shutuma za kutoroka kambini mara kadhaa Kitendo ambacho kilikuwa utovu wa nidhamu na kupewa adhabu ikiwemo kuachwa na kikosini humo.

Pia kwa siku za hivi karibuni klabu ya Simba ilitoa adhabu kwa mshambuliaji wake raia wa Ghana Jonathan Sowah kwa utovu wa nidhamu ambapo mchezaji huyo alishushwa kwenye kikosi Cha vijana U-20 kwaajili ya kufanya mazoezi ikiwa ni sehemu ya adhabu.

Hata hivyo, mjadala mpya umeibuka kufuatia kitendo alichokifanya golikipa wa Yanga, Djigui Diarra, katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliomalizika kwa Yanga kupoteza kwa mabao 3-2.

Katika mchezo huo, Diarra alionekana kususia mchezo baada ya nahodha wa timu hiyo Bakari Mwamnyeto kujifunga bao, kipa huyo aliomba kufanyiwa mabadiliko akishiria kushindwa kuendelea na mchezo na baadae alionekana kwenye benchi akilalamika kutoridhishwa na Kitendo alichokifanya mwamnyeto kwa kujifunga Kitendo kilicho tafsiriwa kama kugomea mchezo.

Wadau mbalimbali wa soka wameendelea kusisitiza kuwa hakuna mchezaji aliye mkubwa kuliko timu, huku wakiamini kuwa nidhamu na mshikamano ndiyo msingi wa mafanikio ya muda mrefu kwa klabu yoyote.

Matukio hayo yanaendelea kuwa somo kwa vilabu na wachezaji kwamba mafanikio ya timu hujengwa zaidi kwa umoja, heshima ya maamuzi ya benchi la ufundi na nidhamu ndani na nje ya uwanja hivyo viongozi wa vilabu wanatakiwa kuhakikisha nidhamu inatekelezwa na kutoa adhabu iwapo Kuna utovu wa nidhamu utakaofanyika ili kuinusuru taswira ya ligi kuu nchini.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments