Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Chelsea FC imefikisha michezo sita mfululizo bila ushindi katika EPL baada ya leo kukubali kichapo cha mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Nottingham Forest, matokeo yaliyo Zima ndoto zao za kushiriki klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao.
Mpaka sasa Chelsea wamejikusanyia alama 48 wakiwa na michezo 35 wakibakiza michezo mitatu kutamatisha ligi huku wakiwa nafasi ya tisa, ambapo hata wakishinda michezo Yao yote iliyosalia watafikisha alama 57 ambazo tayali zimesha fikiwa na Aston Villa aliepo nafasi ya tano.
Katika mfululizo mbaya, Chelsea imefanikiwa kufunga bao moja pekee huku ikiruhusu mabao 14, ikionesha wazi udhaifu mkubwa katika safu ya ushambuliaji na ulinzi, Matokeo hayo yanahusisha vipigo kutoka kwa timu mbalimbali zikiwemo Newcastle United, Everton FC, Manchester City, Manchester United, Brighton & Hove Albion pamoja na Forest.
Kwa sasa The blues wanapambana kushiriki michuano ya Europa wakiwa na machaguo mawili kushinda michezo Yao iliyosalia kujiweka katika sehemu nzuri huku wakiwaombea mabaya wapinzani wao au kushinda fainali ya FA dhidi ya Manchester City ili kupata tiketi ya Moja kwa moja.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment