SOWAH AGOMA KUREJEA SIMBA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji raia wa Ghana na klabu Simba SC, Jonathan Sowah, bado hajaripoti kambini kujiunga na mazoezi ya timu hiyo licha ya uamuzi wa klabu kumrejesha kikosini baada ya kipindi cha kutokuwa sehemu ya timu kutokana na sababu za kinidhamu.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa klabu ilimpa nafasi nyingine mchezaji huyo, lakini ikaweka masharti yatakayomlazimu kuanza mazoezi na kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 kama sehemu ya hatua za nidhamu ili kurejesha utimamu wake wa kimchezo sambamba na kuendana na maadili ya klabu.

Hata hivyo, hadi sasa Sowah hajafika kambini wala kushiriki programu yoyote ya mazoezi iliyoandaliwa na benchi la ufundi, hali inayozua maswali kuhusu mustakabali wake ndani ya kikosi hicho cha Msimbazi.

Bado haijafahamika iwapo kutoripoti kwake kunahusiana na kutoridhishwa na masharti aliyowekewa au sababu nyingine binafsi, huku uongozi wa Simba ukitarajiwa kutoa msimamo rasmi kuhusu hatua zitakazofuata dhidi ya mchezaji huyo.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments