SIMBA KUKUPIGA KMC COMPLEX

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba imetangaza kuhamia Uwanja wa KMC Complex kwa ajili ya michezo yake iliyosalia ya msimu wa 2025/26 baada ya awali kutumia Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kama uwanja wa nyumbani.

Simba tayari ilishawahi kutumia uwanja huo katika baadhi ya michezo yake ya nyuma, huku hatua hiyo ikilenga kuendelea na ratiba ya mwisho wa msimu katika uwanja huo.

Ikumbukwe, uwanja huo ndio unatumiwa na mahasimu wao kama uwanja wao wa nyumbani hivyo Simba wameamua kufuata watani zao huko KMC Complex.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments