Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya AFCON U17 nchini Morocco na kumaliza kinara wa kundi , timu ya Taifa ya Tanzania U17 ‘Serengeti Boys’ imefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia U17 itakayofanyika nchini Qatar mwishoni mwa mwaka 2026.
Katika droo ya hatua ya makundi iliyotangazwa rasmi na FIFA, Serengeti Boys wamepangwa Kundi I pamoja na mataifa ya Brazil, Ireland pamoja na Costa Rica, Kundi hilo linatajwa kuwa moja ya makundi yenye ushindani mkubwa kutokana na historia na ubora wa timu zilizopo.
Michuano ya FIFA U17 World Cup 2026 itaanza Novemba 19 hadi Desemba 13 nchini Qatar, ambapo mataifa 48 kutoka mabara mbalimbali yatashiriki kuwania ubingwa wa dunia ngazi ya vijana.
Serengeti Boys wameandika historia kwa kufuzu michuano hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye AFCON U17, hatua ambayo imeongeza matumaini kwa mashabiki wa soka Tanzania kuona kizazi kipya cha vijana kikifanya vizuri katika jukwaa la dunia.
Hatua hii na matunda ya uwekezaji kwenye soka la vijana kutokana na kuanzishwa kwa Academy mbali mbali pamoja na program za kusaka vipaji kwa vijana ambayo hufanywa na vilabu pamoja na shirikisho la soka nchini.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment