SABABU ZA MADRID KUKOSA MCHEZAJI TIMU YA TAIFA YA SPAIN, BARCELONA WAKITOA NYOTA NANE

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Luis de la fuente ametangaza kikosi cha Spain kuelekea kombe la Dunia, huku FC Barcelona ikitoa jumla ya wachezaji nane walioitwa kujiunga na timu hiyo, wakati Real Madrid ikikosa mwakilishi mmoja, taarifa ambayo imeibua mjadala kutokana na ukubwa wa klabu hizo mbili ndani ya soka la Hispania na mchango wao katika maendeleo ya wachezaji wa taifa hilo.

Barcelona kwa sasa ina jumla ya wachezaji 18 raia wa Hispania ndani ya kikosi chake , huku Madrid ikiwa na wachezaji 12 , tofauti ya wachezaji 6 ambayo imeonekana kuwa sehemu ya sababu iliyochangia Barcelona kutoa idadi kubwa ya wachezaji kwenye kikosi cha Hispania.

Katika miaka ya karibuni Barcelona imeendelea kuwapa nafasi kubwa vijana waliotokana na mfumo wake wa ukuzaji vipaji, hali iliyosaidia wachezaji wengi wa kihispania kupata muda wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza , Kupitia nafasi hizo, baadhi yao wameendelea kuwa sehemu muhimu ya timu ya taifa kutokana na kiwango wanachoonyesha kwenye mashindano ya ndani na kimataifa.

Kwa upande wa Madrid, baadhi ya wachezaji wa Hispania wamekuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha, akiwemo Dani Carvajal. Wengine wamekuwa wakikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kutokana na ushindani uliopo ndani ya kikosi hicho, jambo lililopunguza nafasi zao za kuitwa kwenye timu ya taifa.

Hata hivyo, kutokuwepo kwa mchezaji wa Madrid kwenye kikosi cha Hispania hakumaanishi kuwa klabu hiyo imekuwa na msimu mbaya lakini Mbali na Hispania, Madrid imeendelea kutoa wachezaji wengi kwenye timu mbalimbali za taifa, huku zaidi ya nyota tisa wa klabu hiyo wakitarajiwa kujiunga na mataifa yao kuelekea mashindano ya kimataifa yajayo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments