REKODI YA YANGA YAVUNJWA, DIARA ADAIWA KUSUSIA MCHEZO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Young Africans SC imepoteza rekodi yake ya kutofungwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliochezwa leo katika dimba la Airtel .

Matokeo hayo yameifanya Yanga kupoteza mchezo wa ligi kwa mara ya kwanza msimu huu na kutamatisha mwendelezo wa michezo 42 ya ligi bila kufungwa.

Yanga iliingia katika mchezo huo ikiwa na rekodi ya muda mrefu ya kutopoteza michezo ya ligi tangu ilipofungwa mara ya mwisho na Tabora United msimu uliopita kwa 3-1, na Leo Dodoma Jiji wameuvunja mwiko huo na kuandikisha historia mpya.

Katika mchezo huo, Golikipa wa Yanga Djigui Diarra alifanyiwa mabadiliko kutokana na kuonekana kushindwa kuendelea na mchezo , baadhi ya wadau na mashabiki wanaamini kuwa kipa huyo hakuondoka kutokana na majeraha bali alionekana kuwa na hasira kufuatia bao la kujifunga lililofungwa na Bakari Nondo Mwamnyeto.

Baada ya kutoka uwanjani, Diarra alionekana kuelekea benchi la wachezaji na kuzungumza na baadhi ya wachezaji wa akiba huku akionyesha kutoridhishwa na tukio la kujifunga kwa mwanyeto.

Licha ya kupoteza rekodi hiyo, Yanga bado inaendelea kuwa miongoni mwa timu zinazowania ubingwa wa ligi wakisalia kileleni wakiwa na alama 54 michezo 23.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments