PASI MOJA YA BAO KUMPA UFALME BRUNO EPL

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mei 17, 2026 imekuwa siku ya kihistoria kwa nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes baada ya kufikisha asisti 20 ndani ya msimu mmoja wa Ligi Kuu England na kuingia rasmi kwenye vitabu vya rekodi za EPL.

Kiungo huyo raia wa Ureno sasa ameungana na mastaa wawili waliowahi kutikisa England, Thierry Henry na Kevin De Bruyne ambao pia waliwahi kufikisha idadi hiyo ya asisti katika msimu mmoja wa Premier League.

Bruno aliandika rekodi hiyo kwenye ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Nottingham Forest baada ya kutoa pasi ya bao kwa mshambuliaji Bryan Mbeumo aliyefunga bao la tatu la Manchester United katika mchezo huo.

Sasa macho yote yanaelekezwa kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Brighton & Hove Albion ambapo Bruno anahitaji asisti moja pekee kuvunja rekodi hiyo na kuwa mchezaji mwenye asisti nyingi zaidi kuwahi kutokea katika msimu mmoja wa EPL.

Hii ni fahari iliyoje Kutoka kuwa moyo wa kiungo cha United hadi kuwa mfalme wa pasi za mabao, Bruno Fernandes anaendelea kuthibitisha kuwa ni mmoja wa viungo bora zaidi duniani kwa sasa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments