OLISE AMPIKU MBAPPE TUZO YA MCHEZAJI BORA UFARANSA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Winga wa klabu ya FC Bayern Munich, Michael Olise, ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ufaransa anayekipiga nje ya nchi kwa mwaka 2026 baada ya kuwashinda wachezaji wengine waliokuwa kwenye ushindani huo akiwemo Kylian Mbappe na Rayan Cherki.

Olise ametwaa tuzo hiyo kufuatia kiwango alichoonyesha akiwa na Bayern Munich katika msimu wa 2025/2026, ambapo amekuwa sehemu ya kikosi kilichoshiriki mashindano ya ndani na kimataifa, ambapo katika michezo 50 alizoichezea timu hiyo msimu huu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amehusika kwenye mabao 52.

Takwimu hizo zinajumuisha mabao 20 pamoja na pasi 30 za mabao, hali iliyomuweka miongoni mwa wachezaji waliochangia mabao mengi barani Ulaya msimu huu.

Kutwaa kwa tuzo hiyo kunaongeza mafanikio kwa Olise tangu alipoungana na Bayern Munich, huku kiwango chake kikiendelea kufuatiliwa na wadau wa soka pamoja na wachambuzi wa mchezo huo barani Ulaya.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments