✍️ Rashid Msiri
Mwanakwetu Blog
Katika maisha ya mpira wa miguu, kipaji pekee hakitoshi kumfanya mchezaji adumu kileleni. Wapo baadhi ya wachezaji waliokuwa na vipaji vikubwa sana lakini maisha yao binafsi, hasa changamoto za mahusiano na starehe za nje ya uwanja, yaliathiri maendeleo ya career zao.
Tafiti nyingi dunia zinaonyesha ya kuwa hakuna kiwango rasmi cha asilimia kinachotajwa kuwa kinaharibu maisha ya career za wachezaji kwa sababu kiwango cha mchezaji kinategemea vitu mbalimbali kama vile mazoezi, afya, nidhamu, mazingira ya timu na saikolojia ya mchezaji.
Katika tafiti iliyoongozwa na Bwana Andreas Ivarsson na kuchapishwa kwenye jarida la Journal of Science and medicine in Sports 2020, ulionyesha yakuwa matatizo ya nje ya uwanja haswa mahusiano ya athari ya moja kwa moja kwenye kiwango cha mchezaji haswa katika eneo la kiwango endelevu cha mchezaji kufanya vizuri (consistency) na focus yake katika mchezo kwa muda mrefu .
Inaelezwa ya kuwa kadri msongo wa mawazo unavyoongezeka kwa wachezaji basi na kiwango cha mchezaji husika ndivyo hushuka katika kila mchezo anaoingia kiwanjani hata mazoezi. Imeonekana ya kuwa kwa wachezaji ambao wamekuwa wakipitia matatizo mengi ya nje ya uwanja kumekuwa na correlation ya Hasi -0.48 hadi – 0.67 ya viwango vya wachezaji hupungua kutokana na matatizo binafsi ya nje ya uwanja na msongo wa mawazo.
Yapo majina makubwa ya wachezaji ambao dunia ilishuhudia vipaji vyao na performance zao ndani ya kiwanja kwa muda mfupi huku ikiwaacha watu kuamini ya kuwa wachezaji hao bado walikuwa na vitu Vingi vya kuifurahisha na kuacha historia katika dunia ya soka.
Nani asiye fahamu kipaji alichowahi kuwa nacho Mario Balotelli akiwa Inter Milan na Manchester city ila matatizo ya nje ya uwanja yalikisonga kipaji chake mithiri ya mbegu iliyoota kwenye kichaka cha miba kwani maisha binafsi, starehe, drama za hapa na pale migogoro na wanawake tofauti ya kimahusiano na ubaguzi wa rangi ulisababisha asifikie kiwango ambacho wengi walitarajia akifikie na hii ni hatua ambayo imemfanya aendelee kutajwa kama miongoni mwa wachezaji watukutu duniani, kocha Jose Mourinho aliwahi kusema Mario Balotelli ni moja ya vipaji vigumu kuviongoza.
Wapo wachezaji ambao mahusiano ya ndoa zao yaligeuka kuwa kaburi la vipaji vyao kutokana na changamoto zilizowakuta mfano hai ni Maxi Lopez na mkewe Wanda Nara, story yao ilitikisa sana carrier yake baada ya kuibiwa mke na rafiki yake wa karibu na raia wenzie wa taifa la Argentina Mauro Icard ambaye alimchukua Wanda Nara kutoka kwa Maxi Lopez lakini wa Swahili husema malipo ni hapa hapa duniani kwa mungu ni mahesabu tuuh, Mahusiano ya Wanda Nara na Mauro Icard ambaye alikuja kuwa meneja Wa mchezaji huyo wazamani wa timu ya taifa ya Argentina, timu ya PSG na Inter Milan yaliathiri moja kwa moja mahusiano na vilabu ambavyo alikuwa akivitumikia mchezaji huyo kutokana na drama za wawili hao kwenye mitandao ya kijamii juu ya ndoa yao hali iliyopelekea athari za ndani kwa mchezaji huyo .
Hata hivyo athari za nje ya uwanja hazijaanza kuzungumzwa leo tu, bali ni changamoto ya vizazi na vizazi kutoka soka la ridhaa hadi professional football na hili linaweza kuthibitishwa na moja ya vipaji vikubwa vilivyowahi kupotea na kuacha dunia na maswali mengi juu ya uwezo wake.
Ukipita katika viunga vya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford basi jina la George Best ni moja Kati ya vipaji ambavyo waafizina wa Manchester wanaamini vilipaswa kuandikwa kwa wino wa dhahabu katika majalida ya mchezo wa soka.
Huyu alikuwa mmoja wa wachezaji wenye kipaji kikubwa kabisa duniani. Lakini maisha ya wanawake, pombe na starehe yaliathiri sana career yake. Mpaka leo hutajwa kama mfano wa “kipaji kilichopotea kwa maisha ya nje ya mpira.”
Sio yeye tu pia wapo nyota ambao mazingira ya asili ya kimaumbile ya mwanadamu yaliathiri moja kwa moja maisha yake ya soka na huyu si mwingine bali ni nyota Adriano.
Kwa Adriano haikuwa mapenzi tu, bali changamoto za kihisia na maisha binafsi baada ya kufiwa na baba yake zilimvuruga sana. Pia alikumbwa na mazingira ya starehe na kupoteza focus ya mpira akiwa bado kwenye peak.
Ukiachana na Andriano kwa miaka ya hivi karibuni utakutana na jina la nyota Dele Alli ambaye Watu wengi waliamini angekuwa mmoja wa midfielders bora duniani. Lakini maisha ya nje ya uwanja, pressure za maisha binafsi, pamoja na dhoruba mbalimbali zilianza kuathiri kiwango chake.
Jambo kubwa ambalo limekuwa likionekana kwa wachezaji wengi ambalo limekuwa likipelekea kuanguka kwa carrier zao ni kukosa utulivu wa kiakili pindi wanapopata changamoto za nje ya uwanja, kuzidiwa na hali ya umaarufu mapema na mahusiano yenye drama nyingi , party na starehe nyingi bila nidhamu halisi inayohitajika kwenye michezo hali inayopelekea kupoteza focus kwenye maisha yao ya kimichezo.
Lakini pia si kila changa ya nje ya uwanja na mahusiano yasiyokuwa na afya huharibu career. Wengine huimarika kabisa baada ya changamoto hizo.
Hadithi hizi zinaonyesha kuwa mafanikio ya mchezaji hayatokani na kipaji pekee, bali pia nidhamu, maamuzi sahihi na uwezo wa kutenganisha maisha binafsi na kazi ndio maana makocha wengi wakubwa kama Sir Alex Ferguson, Pep Guardiola na Mourinho wamekuwa wakisisitiza sana nidhamu ya maisha binafsi kwa wachezaji wao.
Haikwepeki ya kuwa Vilabu vina mchango mkubwa sana katika kuimarisha afya ya akili na ustawi wa wachezaji wao, hasa wanapopita kwenye changamoto za maisha binafsi kama mahusiano, presha ya umaarufu, familia, majeraha au msongo wa mawazo.
Ndio maana vilabu Vingi vikubwa kwa sasa vinawekeza kwenye huduma za saikolojia na tiba ya afya ya Akili, kufuatilia maisha ya wachezaji nje ya uwanja na kuweka muongozo mzuri kwa wachezaji vijana kutoka academy ili waweze kuhimili pressure ya umaarufu na changamoto kwenye maisha ya mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa The Football Mental Health Alliance, vilabu vina nafasi kubwa ya kusaidia afya ya akili ya wachezaji na jamii nzima ya mpira kwa sababu vina ushawishi mkubwa kwa maisha ya watu ndani na nje ya uwanja.
Ndiyo maana leo hii kwenye soka la kisasa, afya ya Akili imekuwa sehemu muhimu sawa na gym, mazoezi na lishe kwa wachezaji .
Itoshe kusema katika dunia ya leo ya maisha ya mwanamichezo yeyote afya ya Akili Ina mchango mkubwa katika maisha yake ya kimichezo na kumjenga mchezaji kisaikolojia, kumsaidia asipoteze focus, kumrudisha kwenye kiwango chake pindi anapopitia wakati mgumu nje ya uwanja .
✍🏻 Rashid msiri
Whatsapp 0754645826
rashidmsiri@gmail.com







Post a Comment