Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashabiki wa klabu ya Manchester United wanatarajiwa kutoa heshima kwa aliekuwa mshambuliaji wa Liverpool, Diogo Jota, ( kwa sasa marehemu) kwa kumpigia makofi dakika ya 20 wakati wa mchezo wao wa Mei 3, 2025 katika dimba la Old Trafford
Pendekezo hilo limeripotiwa na mwanahabari David McDonnell, likieleza kuwa wazo hilo limepokelewa na baadhi ya mashabiki wa United, huku uamuzi wa mwisho ukiachwa mikononi mwa mashabiki hao maarufu kama “Red Devils”.
Hatua hiyo inatajwa kuakisi mshikamano katika soka, ikirejea tukio la miaka ya hivi karibuni ambapo mashabiki wa Liverpool waliwahi kumpigia makofi Cristiano Ronaldo katika dimba la Anfield dakika ya saba, kufuatia msiba wa mtoto wake.
Iwapo itatekelezwa, heshima hiyo kwa Jota itakuwa ishara nyingine ya ubinadamu na mshikamano unaozidi kujitokeza ndani ya mchezo wa soka, hata kati ya timu zenye ushindani mkubwa kama United na Liverpool.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment