KUTOKA LIGI KUU TANZANIA BARA HADI KOMBE LA DUNIA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Fiston Mayele ameandika historia nyingine kubwa baada ya kuwa mchezaji pekee anayekipiga ndani ya bara la Afrika kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026 Wakati nyota wengi wa taifa hilo wakicheza nje ya Afrika, Mayele ndiye pekee anayewakilisha ligi za Afrika kwenye kikosi hicho cha ‘The Leopards’.

Nyota huyo wa Pyramids FC ameendelea kuthibitisha ubora wake tangu alipokuwa akiitumikia Yanga Africans, ambapo alijitengenezea jina kubwa kupitia mabao yake na kiwango bora kilichotikisa Afrika , Mafanikio hayo ndiyo yaliyofungua mlango wake kwenda Misri kabla ya sasa kufikia hatua ya kucheza hatua ya juu ya soka Duniani.

Hatua ya Mayele kuitwa akiwa anacheza soka Afrika ni ishara kuwa ligi za Afrika zinaendelea kutoa wachezaji wenye uwezo wa kushindana katika kiwango cha juu duniani. Pia ni sifa kubwa kwa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo iliwahi kuwa sehemu ya safari yake ya mafanikio kabla ya kupanda zaidi kimataifa.

Kwa mara nyingine tena, vilabu vya Yanga Africans na Simba S.C. vinaendelea kuonekana kama daraja muhimu la wachezaji wa Afrika kuelekea mafanikio makubwa duniani, Kupitia majukwaa hayo, mastaa wengi wamepata nafasi ya kuonekana, kuuzwa nje na kufikia hatua ya kuiwakilisha Afrika kwenye jukwaa kubwa la soka duniani.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments