Rashid Msiri
Mwanakwetu blog
Katika miaka ya karibuni, dunia ya michezo imeendelea kushuhudia ongezeko kubwa la majeraha kwa wanamichezo, hasa kwenye soka. Karibu kila msimu, mastaa wakubwa hukosa mechi muhimu kutokana na matatizo ya misuli, magoti, vifundo vya miguu au uchovu wa mwili. Wengine hurudi uwanjani, lakini wengine hawarudi tena kwenye kiwango chao cha zamani.
Hii imeendelea kuibua maswali tofauti tofauti je michezo kwa sasa imekuwa mikali zaidii hadi kufanya miili ya wachezaji kushindwa kuhimili ?
Majera ni moja kati ya adui mkubwa kwa wachezaji kwani wachezaji wengi wenye ndoto kubwa wamewahi kuangushwa sio kwa sababu hawakuwa bora bali ni kutokana na majeraha ambayo yalikuwa yakiwaweka nje ya uwanja kwa muda mrefu sana.
Imekuwa ni hali ya kawaida kwa sasa kusikia wachezaji kuwa nje ya uwanja kwa wiki nne hadi miezi 6 mara nyingi na hii ni kutokana na sababu za majeraha ya ACL, vifundo vya miguu na matatizo ya mgongo.
Hii imekuwa ikiwazui nyota wengi kutokana na kuharibu carrier za wanamichezo hao kwa wakati mmoja mfano wengi wa wachezaji hupitia wakati mgumu kutokana na majeraha kuharibu vitu Vingi kwa mara moja, ikiwa ni pamoja na kiwango chake uwanjani,kujiamini, nafasi yake kwenye kikosi, thamani yake sokoni na kubwa zaidii ni afya ya Akili kutokana na kupitia msongo mkubwa wa mawazo.
Kutokana na tafiti nyingi zimeonyesha sababu kubwa ya majera kwa wachezaji wa kizazi cha sasa ni ratiba nyingi za mechi ambazo husababisha uchovu unao athiri mwili moja kwa moja, mazoezi makali ya mwili ambayo hupelekea shinikizo mkubwa kwenye misuli na viungo, kutopona vizuri jeraha la awali na hii hutokana na wachezaji kuharakisha kurejea uwanjani ili kuendelea kulinda nafasi zao kwenye vikosi wanavyotumikia au rank zao za ubora zisishuke, Lishe duni kwa wachezaji imeonekana ni moja ya sababu zinazowafanya wachezaji kuwa na majeraha ya mara kwa mara ndio maana katika soka la kisasa Kitengo cha nutrition ni moja ya sehemu muhimu katika timu pia wachezaji wengi wakubwa wamekuwa wakiajiri wataalamu wao binafsi wa lishe ili kudhibiti afya zao, viwanja au maeneo mabavu ya michezo pia imeonekana ni moja ya sababu za majeraha kwa wachezaji.
Sababu nyingine ni kukosa huduma nzuri za matibabu, uchovu wa akili, mtindo wa michezo ya kisasa ambao umetoka kwenye kipaji hadi kuwa ni sayansi zaidii hali inayowafanya wachezaji kutumia nguvu kubwa kwenye kukimbia, na pressing nyingi haswa kwenye mpira wa miguu.
Taasisi kubwa za michezo na tafiti za kisayansi zinaeleza kuwa kuongezeka kwa majeraha ya wachezaji kunahusishwa sana na “workload”, ratiba nyingi za mechi, uchovu wa mwili na kukosa muda wa kutosha wa recovery.
Kwa mujibu wa Fifa medical afya na ustawi wa wachezaji ni sehemu muhimu ya maendeleo ya soka, ndiyo maana FIFA imeendelea kusisitiza ulinzi wa afya za wachezaji kupitia tafiti, medical monitoring na injury prevention.
Jarida la kisayansi la Journal of Sports Sciences lilifanya utafiti kwa wachezaji wa academy za kiwango cha juu Ulaya na kubaini kuwa workload kubwa ya wiki kadhaa mfululizo ilikuwa na uhusiano mkubwa na ongezeko la majeraha, hasa kwa wachezaji wa U21. Watafiti walisisitiza umuhimu wa kufuatilia kiwango cha uchovu na mzigo wa mazoezi ili kupunguza majeraha.
Pia utafiti mkubwa wa Sports Medicine kuhusu fixture congestion ulionyesha kuwa kucheza mechi nyingi ndani ya muda mfupi hupunguza recovery time na kuongeza hatari ya kuumia kwa wachezaji wa soka la kulipwa.
Kwa upande wa kisayansi, wataalamu wa sports science wanaamini majeraha mengi hutokea pale ambapo mwili unapewa kazi kubwa kuliko uwezo wake wa kuhimili kwa wakati huo.
Ndoto za wachezaji wengi zimewahi kukatika au kupungua nguvu kutokana na majeraha ya mara kwa mara. Wengine walikuwa tayari wanaonekana kama future Ballon d’Or winners, lakini miili yao haikuweza kuhimili presha ya mchezo wa kiwango cha juu.
Mfano hai ni nyota kama
Marco van basten, mshindi wa tuzo ya ballon d’or mara 3, alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga laki alistaafu mapema kabla ya miaka 30, kutokana na majeraha.
pia yupo Ronaldo Nazario Derima ambae watu wanadai yakuwa isingekuwa kuandamwa kwake na majeraha makubwa ya goti basi dunia ingeshuhudia vitu Vingi kutoka kwake.
Hao ni baadhi tu ya nyota wengi ambao wamekuwa wakitajwa kwa ukubwa kutokana na majeraha yalivyowahi kuharibu kabisa safari yao ya mchezo wa soka.
Ili wachezaji wadumu zaidi viwanjani kuliko kwenye meza za matibabu, kunahitajika ushirikiano mkubwa kati ya vilabu, makocha, madaktari, taasisi za michezo na wachezaji wenyewe. Afya ya mwanamichezo inapaswa kupewa thamani sawa na ushindi wa uwanjani.
Kwa sababu mwisho wa siku, mashabiki wanafurahia kuona vipaji vikicheza, si kuona mastaa wakimaliza muda mwingi hospitalini kuliko uwanjani.
Rashid Msiri
0754645826 Whatsapp
rashidmsiri@gmail.com






Post a Comment