Rashid Msiri
Mwanakwetu blog
Soka la Afrika limekuwa na mbiringe mbiringe za panda shuka kwa miaka, ila wapo magwiji wachache waliweza kuweka alama katika maisha kabumbu la Afrika .
Hivi umewahi kujiuliza Afrika ni wapi soka lilianzwa kuchezwa au je ni nani klabu gani ni kongwe zaidii barani Afrika kuanzishwa ?
Makala haya yameangazia vilabu vikongwe zaidii barani Afrika ambavyo hadi leo vimeendelea kuwepo kwenye Uga wa kabumbu la Afrika , na hii ni kutokana na ripoti mbalimbali zilizochapishwa kwenye majarida na makala mbalimbali zilizoandika historia ya mchezo wa soka barani Afrika.
Kutoka 1936 queens hadi Sunderland kisha simba sports club hii ni klabu kongwe barani Afrika inayoshiriki nafasi ya 10, kwa ukongwe imejizolea umaarufu mkubwa katika soka la Afrika Mashariki kutokana ndio klabu yenye mataji mengi zaidii ya mabingwa wa Cecafa kwa upande wa vilabu na ndio timu yenye ushiriki mzuri katika michuano ya ligi ya mabingwa na shirikisho barani Afrika kwa miaka ya hivi karibuni.
Vijana wa Afrika kutoka jiji la mzizima ama DAR-ES-SALAAM kwa sasa hawa wamebeba ustaarabu na heshima ya mswahili, 1935 klabu ya soka ya DAR-ES-SALAAM Young Africans ilianzishwa katika mitaa ya jagwani na hadi sasa inashikilia rekodi ya kuwa klabu yenye mataji mengi ya ligi kuu soka Tanzania bara hawa wanashikilia nafasi ya tisa.
Namba nane ni kutoka kwenye taifa Senegal ambapo inatajwa klabu ya soka ya Jeanne d,Arc Dakar ambayo ilibeba utambulisho wa mji mkuu wa taifa hilo kwa sasa Dakar timu hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 1921.
Namba 7,Kutoka Katika taifa lenye historia kubwa katika ukombozi wa siasa za Afrika katika Ukanda wa kiarabu taifa la Algeria hapa mnamo mwaka 1921, klabu ya Mouloudia club d’Alger (MC ALGER) ilianzishwa na hadi sasa imebakia kuwa moja ya vilabu venye historia kubwa kwa soka la Algeria na Afrika kwa Ujumla.
Al Masry kutokea pale Nchi Misri inashikilia nafasi ya sita kwa ukongwe barani Afrika ikiwa imeanzishwa mnamo mwaka 1920.
Katika nafasi ya tano imeshikiliwa na kla Club Africain kutokea nchini Tunisia ambao hawa ni moja ya timu zenye mashabiki wengi katika soka la Tunisia.
Esperance sportive de tunis, kutokea nchi ya Tunisia imeanzishwa mnamo mwaka 1919 na hii ni moja ya klabu zenye mafanikio makubwa barani Afrika wakiwa ni moja ya vilabu vilivyowahi kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika.
Wakiwa ni mabingwa mara 5 wakombe la klabu bingwa barani Afrika, wanabeba historia ya kuwa ni moja Kati ya vilabu vinavyolitambulusha ustaarabu wa soka la Afrika, hii ni klabu ya soka ya Zamalek kutokea nchini Msiri inashikilia nafasi tatu kwa ukongwe barani Afrika ikiwa wameanzishwa mnamo mwaka 1911.
Wameweka alama kwa vizazi na vizazi, wamekuwa nembo ya namna ya uwekezaji unavyoweza kulipa katika michezo wamebeba historia na urithi wa mafanikio ya michezo katika taifa la Misri, 1907 klabu ya Al ahly ilianzishwa na kuwa moja ya vilabu vikubwa barani Afrika hadi sasa kwani wanaendelea kuwa mabingwa wa kihistoria wa michuano ya vilabu barani Afrika.
Na timu ya kongwe ya kwanza ni Gezira club kutokea taifa la Sudan imeanzishwa mwaka 1882, na hawa ndio wanasimama kama timu maarufu na yenye ushawishi mkubwa kwa soka la Sudan.
Rashid Msiri
rashidmsiri@gmail.com
0754645826






Post a Comment