INIESTA AANZA UKURUSA MPYA KAMA KOCHA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Andres Iniesta ameanza rasmi maisha mapya ya ukocha baada ya kuripotiwa kusaini kazi yake ya kwanza kama kocha mkuu wa klabu ya Gulf United FC ya Dubai, hatua inayofungua ukurasa mpya katika safari yake baada ya kustaafu kucheza soka.

 Kiungo huyo wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Spain anatajwa kuwa tayari ameafikiana na mabosi wa klabu hiyo kwa ajili ya kuanza majukumu mapya ndani ya benchi la ufundi.

Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na mashabiki wengi wa soka duniani, huku wengi wakiamini kuwa falsafa yake ya uchezaji inaweza kuifanya Gulf United FC kupata mwelekeo mpya, Iniesta ni mmoja wa viungo bora kuwahi kutokea katika kizazi chake kutokana na uwezo wake wa kuiongoza timu na kucheza chini ya presha.

Kazi hiyo ya kwanza ya ukocha itakuwa mtihani mpya , lakini pia nafasi ya kuonyesha kuwa uwezo wake haukuishia tu akiwa mchezaji Bali kuonyesha ubora wa mbinu kama mwalimu akiwa katika benchi la ufundi, Wadau wengi wa soka wanasubiri kuona namna atakavyoanza safari yake mpya pembeni mwa uwanja baada ya kuandika historia kubwa akiwa ndani ya dimba.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments