Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, ameibuka miongoni mwa majina yanayopewa nafasi kubwa ya kuinoa timu ya taifa ya Mali kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Tom Saintfiet.
Taarifa kutoka Mali zimeeleza kuwa Shirikisho la Soka nchini humo limeanza mchakato wa kutafuta mrithi wa Saintfiet, ambaye ameondoka baada ya kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili, Hatua hiyo inalenga kujiandaa na michuano ya kimataifa pamoja na kampeni za kufuzu AFCON zijazo.
Inaelezwa kuwa jumla ya makocha 28 waliwasilisha maombi ya kupewa nafasi hiyo, huku kamati ya uteuzi ikifanya tathmini kwa kuzingatia uwezo wa kiufundi, uzoefu pamoja na maono ya maendeleo ya timu ya taifa.
Katika hatua ya mwisho ya mchakato huo, makocha watano walifanikiwa kuingia kwenye orodha fupi akiwemo Ibenge, Hata hivyo, taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa kocha huyo wa Azam FC ameonekana kuwa mmoja wa makocha wenye nafasi kubwa ya kupewa jukumu hilo.
Ibenge anatajwa kuwa na uzoefu mkubwa katika soka la Afrika baada ya kufanya kazi yenye mafanikio akiwa na timu ya taifa ya DR Congo, ambayo aliifikisha hatua ya nusu fainali ya AFCON mwaka 2015 na robo fainali mwaka 2017.
Huku kwa upande wa vilabu kocha huyo anamafanikio baada ya kuingoza As vita kufanya vizuri ligi ya Congo na kufikisha timu hiyo hatua ya fainali klabu bingwa Afrika mwaka 2014, pia amewaongoza Al hilal ya Sudani kufikia hatua ya robo fainali mara kadhaa ligi ya mabingwa Afrika bila kusahau amefanikiwa kuwapeleka Azam kwenye ramani ya soka la Afrika baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza mara baada ya kupewa jukumu la ukocha.
Hivyo, huenda Ibenge akaondoka Azam fc kama atateuliwa kuinoa timu ya Taifa ya Mali kinacho subiriwa kwa sasa ni maamuzi ya mwisho ya shirikisho hilo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment