Rashid Msiri
Mwanakwetu blog
Rio Ferdinand ni mmoja wa mabeki waliobadilisha kabisa namna dunia ilivyowaona walinzi wa kisasa katika mchezo wa soka. Alizaliwa Novemba 7, 1978 jijini London, England, na tangu akiwa mdogo alionyesha kipaji kikubwa kilichompeleka kuanza safari yake ya soka mafanikio ndani ya West Ham United kabla ya kufungua ukurasa mpya Leeds United na baadaye kuandika historia kubwa kubwa baada ya kujiunga na klabu ya Manchester United. Iliyokuwa ikinolewa na kocha sir Alex Ferguson.
Akiwa uwanjani, Rio hakuwa beki wa kawaida. Ulipokuwa ukiona jezi yake ulikuwa umeona ujasiri mithiri ya simba wa mbuga ya tarangile nchini Tanzania, Alikuwa na uwezo mkubwa wa kusoma mchezo, utulivu wa hali ya juu akiwa na mpira pamoja na uongozi uliowapa hofu washambuliaji wengi duniani. Wengi walimuita “Rolls Royce Defender” kutokana na namna alivyocheza kwa utulivu, akili na kiwango kikubwa cha kujiamini.
Wachezaji wengi wakubwa waliwahi kumzungumzia Rio Ferdinand kutokana na ukali wake wa kiulinzi, ujasiri na uwezo wake mkubwa wa kuongoza safu ya ulinzi. Haya ni baadhi ya maneno yaliyotikisa sana kuhusu Rio, Michael Carrick aliwahi kusema “Rio, a Rolls Royce… got the lot, defend, quick, composed beyond belief.”
Michael Carrick Akimaanisha Rio alikuwa beki mwenye kila kitu; kasi, akili, ukali na utulivu mkubwa.) sio yeye Gary Neville aliwahi kusema Rio Ferdinand ndiye beki bora kabisa aliyewahi kucheza naye, Ukali wa Rio Ferdinand haukuwa wa makelele, bali ulikuwa wa akili, ujasiri na uwezo wa kuwazima washambuliaji wakubwa duniani kwa utulivu mkubwa. Ndiyo maana makocha, wachezaji na wachambuzi wengi waliamini alikuwa mmoja wa mabeki bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya soka.
Katika kipindi chake Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson, Rio Ferdinand alishinda mataji kadhaa makubwa ikiwemo Ligi Kuu England, UEFA Champions League na Kombe la Dunia la Vilabu. Alitengeneza ukuta imara wa ulinzi pamoja na Nemanja Vidić, ushirikiano ambao hadi leo bado unatajwa kama mmoja wa mabeki bora kuwahi kutokea duniani.
Moja ya kumbukumbu kubwa zaidi kwa Rio ilikuwa kuiongoza Manchester United kutwaa UEFA Champions League mwaka 2008 baada ya kuifunga Chelsea kwenye fainali iliyochezwa Moscow. Ushindi huo ulimfanya awe sehemu ya kizazi cha kihistoria cha Sir Alex Ferguson.
Katika kipindi chake Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson, Rio Ferdinand alishinda mataji kadhaa makubwa ikiwemo Ligi Kuu England, UEFA Champions League na Kombe la Dunia la Vilabu. Alitengeneza ukuta imara wa ulinzi pamoja na Nemanja Vidić, ushirikiano ambao hadi leo bado unatajwa kama mmoja wa mabeki bora kuwahi kutokea duniani.
Ndani ya Manchester United aliwahi kuwa na ukaribu mkubwa na nyota kama Christiano Ronaldo na Rio Ferdinand waliandika historia kubwa pamoja ndani ya Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson. Wawili hao hawakuwa tu wachezaji wenza, bali walikuwa marafiki wa karibu waliounganishwa na mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja.
Rio Ferdinand alikuwa mmoja wa viongozi wa safu ya ulinzi wakati Cristiano Ronaldo akigeuka kuwa nyota mkubwa duniani. Katika kipindi hicho, Manchester United ilitawala England na Ulaya, huku wawili hao wakishinda mataji mbalimbali ikiwemo UEFA Champions League mwaka 2008.
Mara nyingi Rio Ferdinand amekuwa akimsifia Cristiano Ronaldo kwa nidhamu, kazi kubwa na mentality yake ya ushindi. Rio aliwahi kueleza kuwa Ronaldo alikuwa tofauti hata mazoezini kutokana na namna alivyokuwa akitaka kuwa bora kila siku.
Wawili hao walikuwa sehemu ya kizazi cha dhahabu cha Manchester United kilichokuwa na majina makubwa kama Wayne Rooney, Ryan Giggs, Paul Scholes na Nemanja Vidić. Ushirikiano wao uliifanya United kuwa moja ya timu hatari zaidi duniani kipindi hicho.
Mbali na mafanikio ya klabu, Rio aliitumikia timu ya taifa ya England kwa miaka mingi na kucheza dhidi ya baadhi ya washambuliaji hatari zaidi kuwahi kutokea katika soka la dunia. Umaarufu wake haukutokana na kucheza kwa nguvu pekee, bali akili yake ya mchezo, nidhamu na uwezo wa kuongoza timu katika nyakati ngumu.
Baada ya kustaafu soka, Rio Ferdinand ameendelea kubaki karibu na mchezo huo kupitia uchambuzi wa soka, miradi ya vijana na shughuli mbalimbali za kijamii. Leo hii jina lake linaendelea kuheshimiwa duniani kama mmoja wa mabeki walioweka alama kubwa katika historia ya mpira wa miguu.
Rashid Msiri
0754645826
rashidmsiri@gmail.com




Post a Comment