Hivi ndivyo Mourinho atarejea Madrid

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha raia wa Ureno, Jose Mourinho, ameripotiwa kuweka masharti kabla ya kurejea kuinoa Real Madrid baada ya mawasiliano ya awali kati yake na uongozi wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya michezo, Mourinho anahitaji uhakika wa vipengele kadhaa ili kukubali kurejea katika timu hiyo.

Mourinho anataka mkataba wa miaka miwili, Pia anahitaji kuja na benchi lake la ufundi pamoja na wataalamu wa mazoezi ya viungo atakao wachagua.

Vilevile, anataka mamlaka katika maamuzi ya kikosi, ikiwemo usajili, upangaji wa kikosi na nidhamu ya wachezaji bila kuingiliwa na uongozi wa klabu.

Taarifa zinaeleza kuwa Mourinho ana wasiwasi kuhusu hali ya majeraha ndani ya kikosi cha Madrid na inadaiwa klabu imekuwa na takribani majeraha wengi katika misimu miwili iliyopita.

Aidha, anataka ulinzi dhidi ya mwingiliano wa bodi katika masuala ya kiufundi, ikiwemo uteuzi wa kikosi na uendeshaji wa timu.

Kwa ujumla, uamuzi wa kurejea kwake utategemea makubaliano kati yake na klabu kuhusu masharti hayo.

0767915473

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments