GAMONDI AKUBALI MZIKI WA SERENGETI BOYS, AWAJUMUISHA WAWILI TAIFA STARS

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17(Serengeti Boys) imewashangaza wengi mara baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya AFCON U-17 yanayofanyika nchini Morocco baada ya kutinga hatua ya fainali kwa kwa mara ya kwanza baada ya kuwaondosha Misri kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Serengeti Boys watavaana na Senegal kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa juni 2, 2026 nchini Morocco huku matumaini ya watanzania yakiwa kwa vijana hao ambao wanatarajiwa kuandika historia kubwa iwapo watafaniwa kutwaa taji hilo, ikumbukwe kuwa hakuna timu yoyote kuanzia ngazi ya klabu na timu za taifa ambayo Ilishawahi kutwaa taji la Africa, hivyo vijana wamekabidhiwa imani kuleta kombe la Africa nchini.

Baada ya kufanya vizuri kwa vijana hao, kocha mkuu wa Taifa stars Miguel Gamondi amewajumuisha nyota wawili kutoka kwenye kikosi hicho ambao ni Luqman Mbalasalu na Kassim Juma kwaajili ya michezo miwili ya kalenda ya FIFA dhidi ya Uganda juni 5 na Rwanda juni 9 ,2026 itakayopigwa nchini Morocco, huku vijana hao wakitarajiwa kuripoti kambini baada ya mchezo wa fainali.

Hatua hiyo inaenda kuongeza uzoefu wa vijana hao kuelekea fainali za kombe la Dunia kwa vijana zitakazopigwa nchini Quatar kufuatia kupata michezo migumu yenye ushindani mkubwa pia watapata fursa ya kufanya mazoezi na wachezaji wenye uzoefu zaidi katika soka hivyo watajifunza mbinu mbali mbali za soka zitakazo wasaidia kwenye safari yao kulisaka kombe la Dunia.

Pongezi kubwa ziende kwa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ( TFF) kwa project bora waliyoianzisha kuhakikisha wanapata vijana wenye vipaji hilo limewalipa kupitia mradi wa TDS Pamoja na kuhimiza timu za ligi kuu kuwa na timu za vijana haya ndio matunda ya uwekezaji.

07679125473,

Lugembetimothy01@gmail.com


0/Post a Comment/Comments