Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) linatarajia kuongeza muda wa mapumziko katika fainali ya Kombe la Dunia 2026, hatua inayokuja baada ya majaribio yaliyofanyika kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Klabu kati ya Chelsea FC na PSG ambapo mapumziko yalidumu kwa dakika 24 badala ya dakika 15 za kawaida hatua ambayo inatarajiwa kufanyika kwenye kombe la Dunia.
Kwa mujibu wa taarifa FIFA inapanga kuifanya fainali ya Kombe la Dunia 2026 kuwa na burudani maalumu ya mapumziko katika kipindi Cha kwanza , mfumo unaofanana na ule wa mchezo wa Super Bowl nchini Marekani.
Hatua hiyo ilianza kuonekana katika fainali ya Kombe la Dunia la Klabu 2025 iliyochezwa kwenye Uwanja wa MetLife nchini Marekani, ambapo Chelsea iliibuka bingwa kwa kuifunga PSG mabao 3-0 mbele ya mashabiki zaidi ya 81,000.
Katika mchezo huo, FIFA iliratibu burudani ya mapumziko iliyowahusisha wasanii mbalimbali wa kimataifa jambo lililosababisha muda wa mapumziko kuongezeka.
Ripoti zinaeleza kuwa mabadiliko hayo yanaweza kuathiri wachezaji ambao kwa miaka mingi wamezoea mfumo wa mapumziko ya dakika 15, huku wadau wa michezo wakieleza kuwa muda huo mrefu unaweza kubadilisha kasi ya mchezo, maandalizi ya kimwili pamoja na umakini wa wachezaji kabla ya kipindi cha pili kuanza.
FIFA pia imekuwa ikifanya maboresho mengine kwenye mashindano yake mapya, ikiwemo mfumo wa kuwatambulisha wachezaji mmoja mmoja wanapoingia uwanjani, mtindo unaotumika zaidi kwenye michezo ya Marekani ikiwemo basketball.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment