FAIDA YA ZIARA YA RIO FERDINAND TANZANIA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ziara ya staa wa zamani wa Manchester United na soka duniani, Rio Ferdinand nchini Tanzania imeelezwa kuwa na faida kubwa kwa maendeleo ya michezo, utalii na uchumi wa taifa kwa ujumla, Wachambuzi wa michezo wanaamini ujio wa nyota huyo utaongeza heshima ya Tanzania kimataifa kupitia nguvu ya soka na ushawishi wake mkubwa duniani.

Kupitia mamilioni ya mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii, Rio Ferdinand anatajwa kuwa daraja muhimu la kuitangaza Tanzania kwa ulimwengu, Vivutio maarufu kamba mbuga za wanyama vinaweza kupata umaarufu mkubwa zaidi endapo nyota huyo atavitembelea na kuvionesha kwa mashabiki wake duniani.

Mbali na utalii, ujio wa Ferdinand unaweza kuwa chachu ya maendeleo ya soka la vijana nchini, Wadau wanaamini kupitia uzoefu wake mkubwa katika soka la kimataifa, vijana wengi watanufaika kwa kupata hamasa, mafunzo na motisha ya kuamini kuwa wanaweza kufikia mafanikio makubwa kupitia mpira wa miguu.

Aidha, ziara kama hizi huvutia wawekezaji na wadhamini wa michezo ambao huongeza thamani ya ligi na vilabu vya Tanzania.

Sekta nyingine zinazotarajiwa kunufaika ni biashara za hoteli, usafiri, vyombo vya habari na bidhaa za michezo kutokana na ongezeko la wageni na ufuatiliaji mkubwa wa kimataifa. Wataalamu wa michezo wanaeleza kuwa ziara za mastaa wakubwa duniani huongeza ufuatiliaji wa kimataifa kwa taifa husika na kusaidia kuimarisha mahusiano kupitia michezo na burudani.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments