EPL YATAWALA FAINALI ZA UEFA 2025/2026, YAINGIZA TIMU FANALI ZOTE

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Vilabu vya England vimeingia katika fainali zote tatu za mashindano ya UEFA msimu wa 2025/2026 baada ya Arsenal ,Aston Villa na Crystal Palace kufuzu hatua ya fainali ya michuano hiyo ya Ulaya.

Kwa upande wa, Arsenal , imeingia fainali ya UEFA Champions League ambapo itakutana na Paris Saint-Germain Mei 30, 2026 katika jiji la Budapest nchini Hungary, fainali hiyo itakuwa yakuvutia kutokana na falsafa ya uchezaji kwa timu zote mbili ushambuliaji zaidi kwa PSG na kuzuia kwa Arsenal

Katika UEFA Europa League, Aston Villa imetinga fainali na itacheza dhidi ya SC Freiburg Mei 27, 2026 kwenye uwanja wa Red Bull Arena nchini Germany.

Nayo Crystal Palace , imefuzu fainali ya UEFA Conference League ambapo itamenyana na Rayo Vallecano Mei 20, 2026 katika mchezo wa kuwania ubingwa wa mashindano hayo huko instanbul, Turkey.

Hatua hiyo inaifanya England kuwa taifa lililoingiza timu katika fainali zote tatu za mashindano ya UEFA msimu huu kitu ambacho ni kipimo kuwa ligi hiyo inaushindani mkubwa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments