Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Bruno Fernandes ameandika historia mpya ndani ya Premier League baada ya kuwa mchezaji mwenye assist nyingi zaidi katika msimu mmoja wa ligi hiyo akiwa amefikisha assist 21.
Rekodi hiyo ameiweka baada ya kutoa pasi ya bao na kufunga kwenye mchezo wa Leo wa kufunga msimu dhidi ya Brighton kwenye ushindi wa 3-0 .
Rekodi hiyo imemuweka juu ya mastaa wawili waliokuwa wakishikilia rekodi hiyo ambao ni Thierry Henry na Kevin De Bruyne waliowahi kumaliza msimu wakiwa na assist 20 kila mmoja, Bruno sasa amekuwa mfalme mpya wa pasi za mabao England baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu msimu mzima.
Mbali na rekodi hiyo, Bruno ameumaliza msimu akiwa mchezaji bora wa EPL baada ya kuhusika moja kwa moja katika mabao 30 ya timu yake, akifunga mabao 9 huku akitoa assist 21 zilizoisaidia Manchester United kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 71 na kufuzu mashindano ya UEFA msimu ujao.
Hakika umekuwa msimu bora kwa Bruno Fernandes, ambaye ameonyesha ubora wa kiuchezaji, uongozi na mchango mkubwa ndani ya kikosi chake hadi kuingia kwenye historia ya soka la England.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment