Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, ameendelea kuwa katika kiwango kizuri baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi kwa mara ya nne mfululizo kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mashujaa FC kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
Katika mchezo huo, Chama aliifungia Simba mabao mawili na kuwa mmoja wa wachezaji waliochangia ushindi huo , tuzo hiyo inaongeza rekodi yake ya hivi karibuni baada ya kufanya hivyo pia katika michezo dhidi ya Yanga Africans , JKT Tanzania na Tanzania Prisons.
Kwa takwimu za msimu huu, Chama sasa amefikisha mabao nane na pasi nne za mabao, hatua inayomuweka nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Zambia anabaki nyuma kwa mabao mawili dhidi ya kinara wa ufungaji Feisal Salum "Fei toto" ambaye ana mabao 10 hadi sasa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment