CARRICK KUPEWA MKATABA WA MUDA MREFU KUINOA UNITED

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mwelekeo uliokuwa ukiripotiwa kuhusu hatma ya Michael Carrick sasa umeingia katika hatua ya uhalisia, baada ya mmiliki mwenza wa klabu ya Manchester United, Jim Ratcliffe, kuripotiwa kuidhinisha rasmi uamuzi wa kumuweka kocha huyo ndani ya mipango ya muda mrefu ya klabu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Carrick ataendelea kubaki ndani ya kikosi cha ufundi cha United na tayari amekubali kusaini mkataba mpya ambao utasainiwa ndani ya siku chache zijazo. Makubaliano hayo yanaelezwa kuwa sehemu ya mpango wa klabu kuimarisha uongozi wa kiufundi kuelekea msimu ujao.

Hata hivyo, bado kuna mjadala kuhusu muda wa mkataba huo mpya ambapo Inaripotiwa kuwa Manchester United inazingatia machaguo mawil ambapo mkataba unaweza kuwa hadi mwaka 2028 ukiwa na kipengele cha kuongeza muda au moja kwa moja kuendelea hadi Juni 2029.

Uamuzi huo unatajwa kuwa sehemu ya mabadiliko ya muundo wa uendeshaji ndani ya klabu hiyo, huku uongozi ukilenga kuleta uthabiti wa muda mrefu katika benchi la ufundi. Carrick anabaki kuwa miongoni mwa watu wanaoaminiwa katika mfumo wa kiufundi kutokana na mchango wake wa muda mrefu akiwa mchezaji na baadaye katika majukumu ya ukufunzi ndani ya klabu.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments