Rashid Msiri
Mwanakwetu blog
1982 ikiwa ni tarehe 2 February kumbukumbu zinaonyesha alizaliwa fundi wa kabumbu na moja ya mabeki hatari na nahodha mwenye mafanikio makubwa zaidii ndani ya klabu ya Yanga.
Kutoka katika visiwa vya marashi ya karafuu, sehemu ambayo ustaarabu wa maisha ya binadamu umezaliwa, alizaliwa binadamu mwenye utulivu, na akili kubwa ya mpira na Uongozi haswa katika safu ya Ulinzi, si mwingine ni Nadri haroub Ali ambaye watu walimathibiaha na nyota maarufu kutoka klabu ya Real Madrid, Fabio Cannavaro hali iliyopelekea kuwa maarufu Kama Nadri Cannavaro.
Alianza maisha ya soka huko visiwani Zanzibar akiwa ni kijana Mdogo katika ardhi ya Michezani visiwani Zanzibar, utulivu wake na uwezo wa kujiamini ulifanya moja ya klabu kubwa visiwani humo kuweza kumuamini ndipo Yanga waliweza kumuona na kumpa nafasi ya kujiunga nao mnamo mwaka 2000, lakini kutokana na magwiji waliokuwepo kikosini hapo kwa miaka hiyo ilikuwa ni ngumu kwa yeye kupata nafasi tena akiwa bado kijana Mdogo, ndipo klabu ya Dar-es-salaam Young Africans mwaka 2003 ilimpeleka Malindi huko visiwani Zanzibar huko alipata muda mwingine wa kucheza takribani miaka miwili.
Na mnamo Mwaka 2005 alirudi tena mitaa ya kariakoo ambapo hapo ndio safari yake ya soka la kulipwa iliweza kuinuka nakuwa ni moja ya historia ya dhahabu iliyoandikwa kuhusu nyota huyu .
Msimu wa 2009/10 akiwa katika kiwango chake bora sana Cannavaro alipata nafasi ya kujiunga na miamba kutoka nchini Canada klabu ya soka ya Vancouver whitecaps ambao baada ya mkopo huo kutamatika alireje ndani ya klabu yake ya Yanga.
Nadri Haroub Ali (Cannavaro) ndani ya klabu ya soka ya Yanga anasimama kama mchezaji na aliyewahi kuchukua mataji mengi zaidii akiwa na klabu hiyo ikiwa ametwa mataji 15 akiwa na uzi wa yanga.
Akiwa yanga ametwa mataji 7 ya ligi kuu, 2 klabu bingwa Afrika Mashariki CECAFA, 4 ngao ya jamii na moja kombe la FA vile nguli huyo akiwa nahodha wa yanga ameisaidia Timu hiyo kuingia hatua ya makundi mara mbili ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2016 na 2018.
Cannavaro alistaafu soka mnamo mwaka 2018 , akiwa amecheza takribani michezo 200 akiwa na jezi ya Yanga na Timu ya taaifa ya Tanzania.
Kila mchezaji huwa na mpinzani wake wa karibu kiwanjani ambaye huwa anaheshimu uwezo wake kwa muda wote moja kati ya historia kubwa kwa nyota huyu ni tukio la nyota wa Timu ya taifa ya Cameroon, klabu ya Barcelona na Inter Milan Samuel Etto aliwahi kuhitaj mabadilishano ya jezi na mchezaji huyo na moja kati ya mahojiano aliyowahi kufanyiwa nyota huyo aliwahi kusema “Nimekutana na washambuliaji wengi wazuri lakini binafsi yangu Walionisumbua ni Samuel Etto wa Cameroon, Didier Drogba, na Hauna Moshi Boban wa Simba “
Cannavaro anaendelea kusimama kama mmoja ya wachezaji na manahodha mahiri kutokea nchini Tanzania kutokana na uwezo wake wa kuyabeba Matatizo ya timu na wachezaji na kuhakikisha yanafanyiwa kazi bila kuathiri timu kwa Ujumla.
rashidmsiri@gmail.com
0754645826




Post a Comment