CAF kutobadilisha mwamuzi, Ndala Kuchezesha Fainali ya CAFCL

 

Timothy Lugembe

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limethibitisha kuwa mwamuzi Jean-Jacques Ndala atasimamia mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mamelodi Sundowns na AS FAR Rabat utakaochezwa Mei 15, 2026 jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Uamuzi huo umefikiwa licha ya malalamiko yaliyoibuka katika siku za karibuni kuhusu uteuzi wa mwamuzi huyo kwa mchezo huo wa fainali ya mashindano ya CAF.

CAF imeeleza kuwa hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwenye jopo la waamuzi lililotangazwa awali, huku ikieleza kuwa imepitia hoja zilizowasilishwa kabla ya kufikia uamuzi huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shirikisho hilo limeendelea kuonesha imani kwa mwamuzi huyo kutoka DR Congo kutokana na uzoefu wake katika michezo ya kimataifa .

Wakati huo huo, mchezo wa mkondo wa pili wa fainali hiyo unatarajiwa kuchezwa Mei 24, 2026 jijini Rabat, Morocco, ambapo bingwa wa msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika atapatikana baada ya matokeo ya michezo yote miwili.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments