Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kiungo wa kimataifa wa Ureno, Bernardo Silva, anatajwa kuwa na nia ya kujiunga na klabu ya FC Barcelona mara baada ya kumaliza mkataba wake na Manchester City msimu huu wa joto.
Kwa mujibu wa ripoti , Silva anatarajiwa kuwa mchezaji huru, akihitimisha safari yake ya mafanikio ndani ya miaka tisa akiwa Manchester City, ambapo amefanikiwa kutwaa jumla ya mataji 18 ikiwemo Ligi Kuu England na michuano ya Ulaya.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 hana mpango wa kuhamia nje ya bara la Ulaya, akipuuza uwezekano wa kucheza ligi za Saudi Arabia au United States. Badala yake, anataka kuendelea kucheza katika kiwango cha juu barani Ulaya kwa misimu michache ijayo.
Inaelezwa kuwa Silva kwa sasa anasubiri uamuzi kutoka kwa mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco, ambaye anatakiwa kufanya marekebisho ndani ya kikosi ili kufungua nafasi ya usajili wake.
Hata hivyo, iwapo dili hilo halitafanikiwa, klabu ya Juventus ya nchini Italy imeripotiwa tayari kuwasilisha ofa ya kumhitaji nyota huyo.
Hatua ya Silva inaweza kuwa moja ya usajili mkubwa wa majira ya joto, huku hatma yake ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka barani Ulaya.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment