Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mabingwa wa Hispania, FC Barcelona, wanadaiwa kufikia makubaliano binafsi na winga wa Newcastle United, Anthony Gordon, katika hatua kubwa ya kuelekea usajili wa majira ya kiangazi.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa nyota huyo tayari amekubali kujiunga na Barca huku mazungumzo rasmi kati ya klabu hizo mbili yakiendelea kwa lengo la kukamilisha dili hilo haraka iwezekanavyo.
Barcelona inaelezwa kuwa inataka kuharakisha usajili huo kabla ya vilabu vingine vya England pamoja na FC Bayern Munich kabla havijaingia rasmi kwenye mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kushambulia kutokea pembeni.
Anthony Gordon amekuwa mmoja wa wachezaji waliovutia zaidi ndani ya Ligi Kuu England kutokana na kiwango chake bora akiwa Newcastle, jambo lililoifanya Barcelona kuona anaweza kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji msimu ujao.
Iwapo dili hilo litakamilika, Gordon ataungana na mastaa wengine vijana ndani ya kikosi cha Barcelona kinachoendelea kujengwa kwa ajili ya ushindani wa ndani na kimataifa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment