BALAA LA MWANAMKE NDANI YA BUNDERSLIGA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Alifukuzwa kocha mwanaume baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabovu Hali iliyo onekana kuzamisha ndoto za timu, busara na imani za kuinusuru timu ziliwekwa mikononi kwa kocha mwanamke ili kumalizia msimu na kuhakikisha klabu ya Union Berlini inasalia kwenye ligi.

Merie Louise Eta amekuwa kocha mwanamke wa kwanza kuongoza timu ya wanaume kwenye ligi tano kubwa barani ulaya, mkataba wake ulianza mwezi April, 2026 baada ya klabu kumuachisha kazi aliekuwa kocha wa klabu hiyo Steffen Baumgart na ikiwa imesalia michezo mitano Marie Eta alikabidhiwa mikoba kwa mkataba wa kumalizia msimu na kuhakikisha klabu inasalia kwenye ligi.

Katika michezo mitano aliyoniongoza timu hiyo ameshinda michezo miwili , sare Moja na kapoteza michezo miwili, katika michezo hiyo alipata ushindi mara mbili dhidi ya Augsburg 4-0, na 3-1 dhidi ya mainz na kumfanya kuwa kocha mwanamke wa kwanza kushinda mchezo ndani ya ligi tano bora barani Ulaya.

 Kabla ya nafasi hiyo alikuwa kocha wa timu ya vijana ya U19 pamoja na kocha msaidizi ndani ya klabu hiyo .

Mbali na ukocha, Eta pia aliwahi kuwa mchezaji wa soka nchini Ujerumani na aliwahi kutwaa UEFA Women’s Champions League akiwa na Turbine Potsdam mwaka 2010 kabla ya kuhamia kwenye taaluma ya ukocha.

Kupitia utulivu wake, nidhamu na uwezo wa kiufundi, Marie-Louise Eta ameanza kubadilisha namna dunia inavyolitazama soka la wanawake, huku wengi wakiamini kuwa huu unaweza kuwa mwanzo wa enzi mpya kwa wanawake ndani ya ukocha wa soka la wanaume.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments